SABABU ZINAZOFANYA WAFUGAJI/WAJASIRIAMALI WENGI, KUSHINDWA KUFIKIA MALENGO?
Watu Wengi wanakimbilia ufugaji/kilimo baada ya kuona majirani na marafiki zao wamepata mavuno bora na yenye faida. Watu wa aina hii hawatengi muda wao wa kujifunza kuhusu mienendo ya soko na mahitaji na uzalishaji wa bidhaa na mazao ya mifugo.
Ufugaji unahitaji uvumilivu, watu wengi hukosa uvumilivu na kutaka mafanikio ya muda mfupi,Kutaka sana mradi ambao unakukidhi kipato cha papo hapo. Wanataka kuwa mamilionea wa muda mfupi. Wafugaji wengi Hawataki kukabiliana na tatizo la udhibiti wa magonjwa ya mifugo au changamoto ya soko. Wafugaji wa aina hii wanachotaka wao ni faida zaidi na zaidi.
Ni muhimu tukafahamu kuwa mafanikio ya ufugaji hayapatikani kwa njia kama hiyo, na usipokuwa makini unaweza kufanya kazi na kujifurahisha tu. Hakuna kitu kizuri kinachokuja kwa urahisi. Ni lazima kufanya kazi kwa bidii na kufanya ufugaji kama ajira.
Hii imekuwa ni changamoto kubwa kwenye miradi ya ufugaji. Gharama za uendeshaji/uzalishaji wa mifugo na bidhaa za mifugo zimeongezeka sana kutokana na bei ya chakula na vifaa muhimu. Inakadiriwa kuwa Zaidi ya 70% ya gharama za uzalishaji zinatokana na chakula cha mifugo. Kutokana na hali hii ReSta AgroVET tunawashauri wakulima kutumia ubunifu na kuboresha vitu hivi ili kupunguza gharama za uzalishaji, kwa mfano kwenye vinywesheo na vilishio mfugaji unaweza kutumia ndoo, makopo au mbao badala ya kununua vifaa vya bei kubwa.
Hii hupunguza kasi ya ufugaji lakini pia huvunja moyo wa mfugaji anayefuga kwa tija. Inavunja moyo sana kumuona mfugaji mwenzako anajitahidi kufanya mradi wa ufugaji kwa kutumia nguvu nyingi na muda mwingi na Kujikuta anaishia kukutana na soko lisilokidhi mahitaji yake na kuuza kwa bei ya hasara asiyotarajia.
Wafugaji wengi wanapokosa mtaalam mwenye taaluma husika kwa ajili ya usimamizi wa mradi wa ufugaji, hujikuta wanaishia kufuga kwa majaribio, makosa na gharama kubwa kisha kushindwa kufikia malengo. Kwa sababu hii wanaishia kuwakatisha tamaa wenzaona hawawezi kupambana na changamoto kama vile magonjwa ya mifugo na wanapoteza kipato kikubwasana.
Tunaweza kuwa tunawataalamu wa mifugo wengi sana lakini hatuwatumii ipasavyo ili kuongeza tija kwenye ufugaji.
Ni hasara kubwa sana inayotokana na ujuzi usio sahihi juu ya uwezo wa kudhibiti magonjwa ya mifugo. Wafugaji/wakulima wengi hawana mazoea ya kufuata ratiba ya mipango ya chanjo na njia za usalama (bio security) na kusababisha vifo vingi vya mifugo na gharama kubwa za matitabu ndani ya muda mfupi. Wafugaji wanapaswa kutumia wataalam wa uhakika na kuepuka vishoka wanaochangia katika uharibifu wa mradi wako wa ufugaji.
Wafugaji wengi hawana taarifa sahihi juu ya mwenendo wa soko la bidhaa za mifugo, na wamekosa ujuzi juu ya mbinu sahihi za kulihudumia soko, hivyo wengi hufuga kwa kubahatisha hali ya soko na wengine huwatumia madalali wakati wa kutafuta soko na mauzo. Pia soko zuri linahitaji uwezo wa kulihudumia wakati wote na kwa ubora ule ule. Wafugaji wengi huweza kuhudumia soko kwa kipindi Fulani na kuna wakati wanaishiwa na bidhaa, hii inasababisha kupoteza uaminifu wa kulihudumia soko.
KUPOTOSHWA NA WAFUGAJI WENZAKE.
Baadhi ya wafugaji wenyewe kwa wenyewe hutengeneza uadui katika ushindani, japo ni kweli kwamba baadhi ya wafugaji wengi wana uzoefu katika ufugaji lakini wengine wanataka kupata mafanikio wao tu. Kwa kutumia nafasi hiyo wanaweza kukudanganya endapo utawauliza wanafanyaje hadi wanafanikiwa?
Pia mfugaji mwingine anaweza kuwa na nia njema na wewe akakushauri vizuri lakini kuna tofauti sana kati mnyororo mzima utakaopitia katika ufugaji hivyo wenda aliyokushauri yasifanye kazi kwa mfugaji asiyekuwa na ujuzi. Ni vema kushauriana na mtaalamu utakuwa ili kuepuka hasara kubwa. ReSta AgroVET Tunawashauri wafugaji kuchukulia ufugaji kama taaluma na kuacha kutarajia mafanikio bila kutumia taaluma.
ReSta AgroVET TUNAWASHAURI WAFUGAJI WA KISASA KUBADILIKA NA KUACHANA NA UFUGAJI WA KIZAMANI USIOKUWA NA FAIDA KUBWA
Wafugaji wanaweza kufanya hivi;
1.) Tafuta ushauri kutoka kwa wataalamu wenye taatuma husika. Wafugaji wenye uzoefu wanaweza kuwa wa msaada kwako lakini mtaalamu atakusaidia kuwa na mafanikio zaidi. Mitandao ya kijamii inaweza kusaidia wafugaji kununua au kuuza bidhaa zao na kushiriki katika kutoa mawazo na changamoto lakini ni lazima ielewe kuwa kuwa, mfugaji makini hafanyi ugunduzi na matibabu ya magonjwa kwa online (Achana na Vishoka pata, huduma ya uhakika). Ni vizuri Mtaalam wa mifugo atembelea shamba lako na kutoa huduma.
2.) Daima tafuata taarifa sahihi za soko na masoko ya bidhaa/mifugo yako kabla ya uzalishaji na kabla ya kufikia muda wa kuuza bidhaa zako. e.g nyama na mayai. Maarifa ni muhimu.
3.) wafugaji wajitahidi Kupunguza gharama za uzalishaji kwa kadri iwezekanavyo kwa kutumia bidhaa nafuu lakini zenye ubora wa juu.
4.) Jitahidi kwenda semina na mafunzo ya ufugaji kwa kila wakati unapopata fursa. Hii itakusadia kufahamu mambo mengi Zaidi na teknolojia na mbinu mpya zinazotumika kwenye ufugaji. Kupata maarifa hakukuletei hasara bali hukupa faida. Wafugaji wengi hupotezwa na wafugaji wenzao na vishoka wanaopatikana kila kona. Jitahidi kupata maarifa kwa sana na kuwa karibu na mtaalamu wa mifugo wa uhakika na aneaminika
5.) Pata mifugo kuanzia mradi kutoka kwenye Chanzo kinachoaminika na kuthibitika. Kwa kutumia msaada wa mtaalam mfugaji unaweza kufahamu aina nzuri ya mifugo unayohitaji, na kujua historia ya vizazi vilivyopita kizazi hadi kizazi, ubora wa uzalishaji na kiwango chake. Epuka inbreeding yani kuzalisha kizazi cha ukoo mmoja mara nyingi Zaidi ya kizazi cha tatu hupunguza ubora na kusababisha, udumavu na mwishoni uzalishaji uliopungua.
SOMA FUGA TIMIZA MALENGO
IMEANDIKWA NA Dr RIZIKI NGOGO (VET)
ReSta AgroVET
0763222500/ 0652515242
www.afyamifugo.wixsite.com/agrovet
Tanzania.